Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas (kushoto) akimkabidhi mfano wa Hundi ya shilingi Milioni 521,471,360, mshindi wa awamu ya sita wa Jackpot, Abdulazizi M Ibrahim, baada ya kuibuka kidedea.
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri SportPesa leo Aprili 9, 2021 imemkabidhi rasmi mshindi wa awamu ya sita wa Jackpot mfano wa hundi ikiwa ishara ya kutimiza wajibu kama kampuni kwa washindi wake.
Mkazi wa Tabora-Sikonge Abdulaziz Ibrahim, (24) ambaye pia ni mwajiriwa wa duka la dawa na maabara amekabidhiwa na SportPesa pesa aliyoshinda Jackpot ya mechi 13. Wakati wa makabidhiano katika ofisi za SportPesa Abdulaziz alisema “Nafurahi sana kwani baada ya kusubiri kwa kipindi kilichopangwa leo (jana) nimekabidhiwa rasmi fedha zangu.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas wa kwanza kushoto, akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Jackpot ya Sportpesa, Abdulazizi Ibrahim, pamoja na baadhi ya wachezaji wa Simba na Yanga waliohudhuria makabidhiano hayo.
“Napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza maana nilishajaribu mara kadhaa lakini sikufanikiwa.
“Siku niliyoshinda niliweka mikeka kumi na kila mmoja shilingi elfu mbili, katika mikeka yote 10 mkeka namba 7 ndio niliofanikiwa kushinda kwa mechi zote.
“Mimi ni shabiki mkubwa wa Manchester United na kwa hapa Tanzania nashabikia Young Africans. Siku niliyoweka mikeka yangu niliikosesha ushindi Man U ambayo ilikuwa inacheza na Leister City kupelekea kufanikisha vizuri ushindi wangu,” alisema Abdulaziz.
Mchezaji wa Simba Miraji Athuman (kushoto), akiwa katika pozi na mshindi wa Jackpot ya Sportpesa, Abdulazizi Ibrahim, muda mfupi baada ya kukabidhiwa hundi hiyo.
Kwa upande wa SportPesa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas alianza kwa kuwashukuru Waandishi wa Habari kwa kuhudhuria tukio hilo muhimu la kumkabidhi mshindi mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360 na kusema kuwa;
“Leo ni siku ambayo tulikuwa tunaingojea kwa hamu sana maana tumeweza kukamilisha hili zoezi, huyu mshindi alipatikana tangu tarehe Machi 22, mwaka huu lakini ilibidi tusubiri kipindi hiki cha maombolezo kimalizike ndipo tuendelee na sherehe ya kumkabidhi.
Mshindi wa awamu ya sita wa Jackpot ya Sportpesa, Abdulazizi Ibrahim akiwa ameshikiria mfano wa hundi baada ya kukabidhiwa mapema leo kwenye ofisi kuu za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
“Katika ushindi wake Abdulaziz ameweza kubaki na Shilingi 417,177,488 huku akitoa Shilingi 104,293,872 kama malipo ya kodi ya zuio.
“Lengo letu ni kuendelea kuwainua vijana Wakitanzania na kuhakikisha tunabadilisha maisha yao, kwa kucheza jackpot tumeweza kuona jinsi Abdulaziz anavyoenda kubadili maisha yake.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa kwenye pozi na mshindi wa Jackpot ya Sportpesa, Abdulazizi Ibrahim muda mfupi baada ya kukabidhiwa hundi yake.
“Kila siku tunaendelea kuwa wabunifu ili kuhakikisha tunaboresha huduma na kuwafanya wateja wetu wazidi kufurahia kucheza na SportPesa.
“Hivi sasa Jackpot yetu imepanda upya na kufikia kiasi cha shilingi TZS 218,361,140 ambapo kwa atakayebashiri kwa usahihi mechi 13 ataibuka mshindi na kwa watakaobarishi kwa usahihi kuanzia mechi 10 hadi 12 watapata bonasi ya wiki.
“Endapo Jackpot haitopata mshindi kwa wiki hiyo huongezwa mpaka pale mshindi atakapopatikana,” alisema Tarimba.
0 Comments