Meneja wa Masoko wa Parimatch, Bwana Levis Paul akizungumza na waandishi wa habari.
 
Kampuni ya Michezo ya Kubashiri Parimatch kwa kushirikiana na Mtandao wa Tigo Pesa leo inazindua rasmi promosheni yake mpya ya ‘VIBUNDA SPESHO’, Kampeni yenye lengo mahsusi kuwazawadia wateja wetu fedha kila siku na wiki, hii ikiwa ni kuelekea maandalizi ya sikukuu za Chrismas na mwaka mpya.
Kampeni hii ni mahususi kwa wateja wote wa Tigo Pesa na Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi cha kuanzia Novemba 06. 2023 hadi Disemba 06. 2023.

Hayo yamebainishwa na Meneja Masoko wa Parimatch, Bwana Levis Paul na kusema kuwa mara baada ya kufanya maboresho makubwa katika tovuti yao kwa kuwapa wateja wao PARIMATCH JACKPOT sasa hivi wameamua kuwajaza vibunda ili wazidi kuburudika pindi wanapokuwa wanasuka mikeka yao na Parimatch.
“Mteja wa Parimatch akifanya bashiri kwenye mchezo wowote kupitia www.parimatch.co.tz atakuwa na fursa ya kushinda zawadi ya Tsh. 50,000/- (Elfu Hamsini) kila siku na kila mwisho wa wiki yaani siku ya Ijumaa kutakuwa na droo kubwa ya kumtafuta mshindi wa zawadi ya Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-) ambayo itakuwa inaoneshwa mubashara kupitia runinga ya TBC”, alisema Levis.

Meneja Biashara wa Kampuni ya Tigo Pesa, Fabian Felician akifafanua kuhusiana na ushirikiano huo.
Kwa upande wake, Meneja Biashara wa Kampuni ya Tigo Pesa, Fabian Felician amewahimiza wateja wa mtandao huo kuchangamkia fursa kupitia promosheni hiyo ambayo wanashirikiana na Parimatch.

“Wateja wa mtandao wa Tigo Pesa wanaweza kupata zawadi hizo kupitia Parimatch kwa kusuka mikeka yao kwenye tovuti pamoja na App ya Parimatch mara tu unapojisajili endapo ni mteja mpya na kwa wale wenye akaunti tayari watapaswa kuingia ili waanze kusuka mikeka yao na kusubiria ushindi wao,” alisema Fabian