Kuweka na kutoa Pesa 1xbet kwa njia ya bank na skrill

Niaje wazee wezangu wa mikeka?

Hivi karibuni kumekuwa na changamoto kubwa ya kuweka na kutoa pesa katika mitandao ya 1xBetMelbet na Betwinner kwa njia watu wengi tuliyokuwa tumeizoea ya Mobile Payment (M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money). Tatizo hili limekuwa likijirudia mara kwa mara na kusababisha adha kubwa kwa wadau wa mikeka.

Kupitia post hii nawapa ujanja wazee wenzangu wa mikeka ni jinsi gani unaweza kuweka fedha na kutoa katika makampuni hayo wakati bado tunaendelea kusubili njia za kuweka kwa Mobile Payment zikae sawa.

Kuna njia nyingi unaweza kutumia ukiachana na hiyo ya Mobile Payment, lakini kufuatia njia hizo kuonekana zina mlolongo mrefu na ugumu kidogo leo nitawaelekeza njia mbili ambazo kwa upande wangu nimeona kwamba ni rahisi kuzitumia. Njia hizo ni:

1. Kadi ya Benki (Bank Card)
2. Skrill

KADI YA BENKI (BANK CARD)

Njia hii ni kwa kutumia njia ya kadi yako ya benki (wengi wamezoea kama ATM Card) unaweza kuweka na kutoa pesa moja kwa moja katika akaunti yako kwenye makampuni hayo. 
Lakini unapotumia kadi yako ya benki kwa benki kama NMB, CRDB, na nyinginezo unatakiwa kufika katika tawi la benki yako na kuwaomba waruhusu kadi yako iweze kutumika kufanya malipo mitandaoni (online payment).
Kwa benki kama Banc ABC na UBA wao unaweza kuomba kupewa kadi peke yake bila ya kuwa na akauti katika benki zao na kadi hiyo moja kwa moja inakuwa tayari kutumika kufanya malipo yoyote mitandaoni. Pia kupata kadi hizo ni rahisi kwani si zaidi ya nusu saa unakuwa umepewa kadi yako. Pia kadi hizo unaweza kuziwekea pesa kupitia matawi yao ya benki au kupitia M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money na pia unaweza kutoa pesa katika ATM ya benki yoyote.

Changamoto kubwa katika njia hii ya kadi ya benki ni kwamba unapotaka kutoa pesa yako katika account yako ya 1xBet, Melbet au Betwinner lazima kianzie kiasi cha Tshs. 130,000/=.

SKRILL

Njia hii ni kupitia kampuni hii ya Skrill inayotumika kufanya malipo mitandaoni. Unachotakiwa kufanya ni kufungua akaunti yako katika kampuni hii ya skrill (bofa hapa www.skrill.com). Ukiishafungua akaunti yako skrill unaweza kuiwekea pesa kupitia kadi yako ya benki na kisha kupitia akaunti yako ya skrill ukaweka na kutoa pesa katika makampuni hayo ya kubet. Lakini angalizo ni kwamba ili uweza kuitumia akaunti yako ya skrill bila ukomo wowote inatakiwa account yako iwe verified (imehakikiwa). Fuata hatua za verification ambazo zimewekwa na hapa mara nyingi wanataka uhakika wa taarifa zako hivyo utatakiwa kuscan ID yako na kuiupload na pia statement yako ya kibenki kuhakiki anuani yako au document yoyote utakayoona inafaa kulingana na chaguzi zitakazokuwepo (utapata maelekezo hapo hapo kwenye akaunti yako ni nini kinatakiwa kuwa verified).

Akaunti yako ya skrill isipokuwa verified utaweza kutuma na kupokea pesa kiasi fulani ambacho kitakuwa kimewekewa ukomo. Faida mojawapo ya kuwa verified ni kwamba kunakuwa hakuna ukomo wa kuweka na kupokea pesa na kwamba pia unaweza kutoa pesa yako kwenda kwenye akaunti yako ya benki moja kwa moja.

Bofya HAPA kujiunga na 1xbet

Post a Comment

1 Comments

  1. Nimekuelewa Mzee lakin mimi nna changa moto ktk kutumia app hii kama unauzoefu nayo tafadhar msaada wako mkuu 0625 858581 maana siielewi kbs sportpesa na mbet ndo nazitumia sana

    ReplyDelete