Rais wa Yanga Injnia Hersi Said akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tarimba Abbas Tarimba

KLABU ya Yanga imeingia makubaliano na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.033 ambao utakuwa ni wa kipindi cha miaka mitatu (3).

 

Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tarimba Abbas Tarimba amesema Kampuni ya Sportpesa ndiyo Kampuni pekee ya michezo ya kubashiri iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kusaidia vilabu vya Simba na Yanga kujiimarisha kiuchumi kupitia udhamini wao lakini pia kupitia mashindano ya Sportpesa tangu mwaka 2017.

Tarimba amesema SportPesa ndiyo Kampuni ya kwanza nchini Tanzania iliyoweza kuvisaidia vilabu vya Yanga na Simba kujiimarisha kiuchumi tangu mwaka 2017

Aidha Tarimba amesema Klabu ya Yanga itanufaika na Mkataba huu kwenye vipengele kadhaa ikiwemo endapo Klabu ya Yanga itashinda taji la Ligi Kuu ya NBC basi itafanikiwa kunyakua kitita cha Shilingi milioni 150 lakini pia klabu itafanikiwa kunyakua kiasi cha shilingi milioni 75 endapo tu itafanikiwa kufika fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup.


Soma pia >kampuni Bora za kubeti tanzaniaRais wa Yanga Injinia Hersi Said

Kwa upande mwingine Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameipongeza Kampuni ya Sportpesa chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Abbas Tarimba kwa kufikia makubaliano hayo ya kihistoria kwa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani huku akiahidi kusimamia maelekezo na makubaliano ya mkataba huo na kusisitiza kuwa Yanga ipo tayari kufanya mambo makubwa zaidi na SportPesa


Source: globalpublishers.co.tz