DSM: Bodi ya michezo ya kubahatisha (GBT) imeeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 20 imefanikiwa kulinda haki za wachezaji na kutatua migogoro ya wachezaji na waendeshaji wa kampuni za michezo ya kubahatisha na kuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo katika maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake imeeleza kuwa bodi hiyo itaendelea kukuza, kusimamia na kudhibiti sekta hiyo.

Aidha imeeleza kuwa itaendelea kusimamia uadilifu kwa lengo la kuchangia pato la taifa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha ambayo inachangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa.

Pia imeeleza kuwa mchango wa sekta hiyo katika mfuko wa serikali imekuwa kwa kiasi kubwa kwani kwa mwaka 2006/07 mapato yalikuwa Sh bilioni 2.8 lakini kwasasa mapato hayo yameongezeka na kufikia Sh bilioni 170.4 kwa mwaka 2022/2023.

Katika hatua nyigine bodi hiyo imesema kuwa imeendaa mazingira mazuri ya uendeshaji wa sekta ya michezo ya kubahatisha na kuvutia kampuni nyingi zaidi kutoka kampuni tisa mwaka 2003 hado kampuni 53 mwaka 2023.