Tasnia ya michezo ya Bahati nasibu imezidi kuka siku hadi siku kutokana na maendeleo ya teknolojia na mapinduzi ya smart phone, huku ikiwavutia mamilioni ya wachezaji duniani kote. Michezo hii huchukuliwa kama burudani huku ikiwa na nguvu kubwa ya kuathiri akili na uchumi wako kama hutacheza kwa taharari kubwa na kuwa na uwezo binafsi wa kujidhibiti. Katika Makala hii tutajikita katika kukuonesha wakati sahihi wa kuacha kabisa kubeti au kupumzika kwa muda kama ifuatavyo.
Kama unategemea betting au kasino kama chanzo cha mapato; Michezo ya betting ni starehe isiyostarehesha wakati mwingine hivyo haipaswi kuwa kama chanzo chako cha kipato bali kama sehemu ya burudani tu. Hii nikwasababu katika kubahatisha hakuna uhakika wa kipato hivyo kutegemea kama chanzo cha kipato kunaweza kukufanya kupoteza fedha nyingi au kuwa mraibu
Ukigundua huwezi kujidhibiti tena; hatua ya haraka niyakutafuta msaada wa kukusaidia kuacha kubeti kwani upo kiwango kibaya cha uraibu, hali hii utaitambua kwa kila wakati kutamani kucheza, au ukipata fedha kabla ya maamuzi mengine yoyote unaanza kubeti. Ukipitisha siku bila kucheza unaona kama siku yako haijakamilika. Ukifika hapo nimuhimu kuacha au kupiumzika
Umepoteza fedha nyingi kwa wakati mmoja; Hii nit aa nyekundu kuwa unapaswa kuacha kubeti, kwani kuendelea ukiwa na lengo la kurudisha kiasi ulichopoteza unaweza kupoteza zaidi na kukuweka katika halimbaya kiuchumi. Kubali kosa ulilokwisha tent, jisamehe ili uepuke kupoteza zaidi
Unabeti fedha za mahitaji ya msingi ; hali hii huja pale ambapo kila peso itakayopita mkononi mwako kutamani kuichezea ili izalishe faida, madhara yakke ni kwamba unaweza kupoteza fedha hiyo na kukusababishia kuathiri mahitaji yako na kukwama kwa mahitaji yako ya muhimu. Nimuhimu kubeti kiasi cha ziada tu nasio fedha iliyokatika bejeti muhimu.
Hauna bajeti au unavuka kiwango cha mwisho ulichojiwekea katika kubashiri,; Nimuhimu kuwa na kiwango cha mwisho ambapo hutazidi kiwango hicho hata iweje kwamfano unaweza kubeti kwa kiwango cha chini ya asilimia moja ya kipato chako kwa mwezi na hutakiwi kuzidi kiwango ulichojiwekea
Ukiona inakuathiri kufanya mambo ya msingi; kama unapoteza change mwingi katika kuweka Bashiri au kucheza kasino kisha unakosa mud awa kufanya mambo ya msingi kama vile kufanya kazi, kuwahi kazini, kusoma na nk basi unapaswa kuacha au kupumzika haraka sana,
Unaanza kuingia kwenye madeni au kukopa fedha ya betting; Hapa umefika kiwango kikubwa cha kuathirika kiuchumi, sio sahihi kukopa fedha kwaajili ya starehe, kama hauna kiasi cha ziada cha kucheza nimuhimu kupumzika au kuacha kucheza kabisa.
Kama unamatarajio kunna siku utafanikiwa kupitia betting; HHii ni hali mbaya ya kiakili ambayo inaweza kukusukuma na ukapoteza fedha nyingi huku ukiwa na ndito kuwa kuna siku utafanikiwa kupitia michezo ya betting, nikweli unaweza kushinda kiasi kikubwa lakini huwa inatokea mara chache sana na kuna uwezekano wa kushinda na kuanza kupoteza karibu kiasi chote ulichoshinda. Mafanikio huja kwa kufanya kazi na betting ibaki kama sehemu ya starehe tu
NINI CHA KUZINGATIA
Mara zote kumbuka kucheza kistaarabu na kumbuka kuweka kiwango ambacho hutaumia kama ukipoteza. Kwamfano umebetia tsh 100 ningumu wewe kuumia au kujutia pale unapopoteza

0 Comments