SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa beki wa Simba Yusuph Mlipili anatakiwa kuongeza juhudi ili kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Mlipili ndani ya Simba msimu huu hajawa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kutokana na kile kinachoelezwa ni ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Simba.

Kwa sasa Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 imebakiwa na mechi 10 kukamilisha mzunguko wa kwanza ila kwa sasa ligi imesimama kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.

Sven amesema:"Bado kuna nafasi ya wachezaji wasiokuwa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kucheza ikiwa ni pamoja na Mlipili haina maana kwamba ni mchezaji mbaya hapana ni lazima aonyeshe utofauti na wengine kwani kikosi kina wachezaji wengi,".