HERRY Mzozo, meneja wa beki wa kushoto wa Simba, Mhaomed Hussein amesema kuwa mteja wake bado hajasaini mkataba na timu yake hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.
Imekuwa ikielezwa kuwa Mohamed ambaye ni nahodha msaidizi amewekwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ambao wanahitaji kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.
Meneja huyo amesema:"Mohammed hajasaini Simba kwa sasa ila ipo wazi mkataba wake umebakiza miezi miwili hivyo ikiisha hapo tutajua atabaki Simba ama atarudi Kagera Sugar.
"Ni mchezaji mzuri ambaye anafuatiliwa na wengi hivyo nina amini kwamba kipaumbele cha kwanza kwetu sisi ni timu yake ya Simba kisha mengine yatafuata.
"Unajua kwa hatua ambayo Simba imefika na yeye kucheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika wengi wamemuona na wanatambua uwezo wake, kuhusu yeye kwenda Yanga, hakuna ofa niliyopokea," amesema.
Kwenye hatua ya makundi,Simba ikitinga hatua ya robo fainali Mohamed amecheza mechi zote sita za ushindani alianza kikosi cha kwanza.
mkwanja 22Bet is giving you 100% welcome bonus ,click here to register and get the bonus