KITABU CHA FURSA ZA KIDIGITALI CHA ZINDULIWA RASMI

 

Dar es salam,  Kitabu hicho kilichoainisha fursa mbalimbali za kidigitali  kimezinduliwa leo rasmi jijini Dae es salaam

Aidha katika uzinduzi huo nilipozungumza na mwandishi wa kitabu hicho ndg Emanuel ameeleza kuwa kitabu hicho ni kwaajili ya wale wote wanaosaka fursa za kidigitali  katika makundi yote akitaja baadhi ambao ni vijana, wanafunzi, waalimu, wanamuziki, waandishi  pamoja na wafanya biashara.

Akitaja baadhi ya fursa zinazoelezwa katika kitabu hicho mwandishi amesema kuwa katika kitabu chake ameeleza namna mbalimbali za kuuza bidhaa za kidigitali mtandaoni kama vile vitabu (E-books) kuuza muziki mtandaoni, kuanzisha duka mtandao, mbinu za kufundisha mtandaoni, kuuza kozi  na notes mtandaoni,  uuzaji wa maudhui mtandaoni, kuwa freelancer wa kidigital, YOUTUBE, miongoni mwa fursa nyingine za kidigital.

Vilevile amesema kuwa kitabu hicho kimeanza kuwa dukani tangu tarehe 23 ya January  2022. Nakuongeza kuwa kwa wale wanaohitaji kitabu hicho wawasiliane kwa simu  0766605392

Post a Comment

0 Comments