Kama wewe nimchezaji wa michezo ya kubeti na unapita katika mitandao mbalimbali ya kijamii neon fixed game sio neon geni kwako. Wapo watu mbalimbali ambao hujinadi mtandaoni kuwa ni chimbo la fixed game huku wakiuza ods  na wengi wa wateja wao wamekuwa wakiambulia za uso na kuishia kutukana. Katika makala hii tutajadili kwa undani uwepo wa fixed game au correct score na jinsi zinavyoweza kupatikana.

Fixed game ninini? Haya ni matokeo ya mchezo husika yaliyopangwa yani hata iweje lazima mpira uishe katika matokeo hayo. Kuna tofauti kubwa kati  ya predictions/utabiri na fixed game huku utabiri ukiwa ni yale makisio ya namna mchezo unavyoweza kuisha lakini fixed ni matokeo ya moja kwa moja na hayatarajiwi kubadilika.


JE KUNA UKWELI KUHUSU FIXED GAME?

Hakuna jibu la moja kwa moja unaloweza kuwa nalo  kutokana na kuwa hata prediction inaweza kuwa fixed mfano mtu anaweza kutabiri matokeo ya mpira samba vs yanga itaisha 0-0 na ikatokea kuwa hivyo haimaanishi ni fexed, kwani fixed game hughusiha kunaunua mchezo husika na kupanga matokeo. Kwakuwa kunao watu mablimbali wanamichozo waliokwisha kutuhumiwa kwa kupanga matokeo ya michezo basi jibu nikuwa fixed game zipo.

UPATIKANAJI WA FIXED GAME

Upatikanaji wa fixed game ni mgumu na hata ikitokeo umepatikana ningumu kumfaidisha mchezaji wa beti mdogo. Kwakuwa upangaji wa matokeo haukubali hivyo nisiri sana kwa mchakato wa fixed game kufanyika. Hata inapotokea kwa kampuni ya kubeti kugundua kuwa umeweka beti yako kwa kufuata fixed game account yako huweza kufungwa au kutopewa pesa ulizoshinda kabisa. Vilevile kampuni ya kubeti wanapoona stake zinazotia shaka katika mchezo mmoja Fulani mchezo huo huondolewa au odds husika kufungwa. Hivyo utakubaliana name kuwa hata ikiwa fixed ipo katika mchezo Fulani ningumu kuenea au kukufikia ili kukwepa hatari hiyo

Hivyo tunaweza kuhitimisha kuwa nivigumu sana kupata upangaji wa matokeo (fixedgame)  hata kama utaambiwa utoe fedha nyingi kununua. Utakachouziwa ni predictions ambazo zinaweza kwenda kinyume au zikaenda sawia.


SOMA PIA 👉KAMPUNI BORA ZA KUBETI TANZANIA