PARIMATCH YAIDHAMINI MASHUJAA FC

 

Mkurugenzi wa kampuni ya Parimatch Tanzania, Erick Gerald (kushoto) akisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano pamoja na Kiongozi wa timi ya Mashujaa FC, Benjamin Kisinda .

Zikiwa zimesalia takribani siku nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kampuni ya michezo ya Kubahashiri Parimatch imetangaza rasmi kuingia makubaliano ya kuidhamini Klabu ya Mashujaa FC kwa msimu wa
2023/24.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Parimatch Tanzania, Erick Gerald wakati wa zoezi la utiaji sahihi wa mkataba ambao umefanyika leo katika ukumbi wa ofisi za Mashujaa fc baina ya Uongozi wa Kampuni hiyo mbele ya vyombo mbalimbali
vya habari.
Aidha Erick amesema lengo mahususi ya mkataba huo ni kukuza soko la mpira nchini pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
Parimatch tumekuwa wadau wakubwa kwenye sekta ya michezo hapa nchini na nje ya nchi na kupitia udhamini huu unalenga kusaidia timu ambayo ina vijana wanaopata ajira, wanajenga afya na kuleta ushindani kwenye michezo",
amesisitiza Erick.

Mkurugenzi wa kampuni ya Parimatch Tanzania, Erick Gerald (kushoto) akionesha mkataba wa makubaliano ya ushirikiano pamoja na Kiongozi wa timi ya Mashujaa FC, Benjamin Kisinda .

Kwa upande wake kiongozi wa timu ya Mashujaa FC, Benjamin Kisinda ameishukuru Kampuni ya Parimatch Tanzania kwa kuwaamini na kuwaunga mkono katika udhamini huo ambao utawasaidia kupunguza changamoto za uendeshaji wa klabu.
“Tunawashukuru wadhamini wetu Parimatch kwa kuja kuungana nasi katika kuendeleza soka, Mashujaa ni timu ambayo imepanda daraja msimu huu, kwa hivyo tunawakaribisha sana Kigoma katika familia ya Mashujaa”, amesisitiza
Kisinda.

Post a Comment

Previous Post Next Post