SPORTPESA NA TIGO WAZINDUA KAMPENI YA “MAOKOTO, DEILEE”

Promosheni hii inawapa wateja wa Tigo pesa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kwa kuweka pesa kupitia huduma ya TigoPesa na kubashiri michezo waipendayo SportPesa.

Dar es Salaam, Agosti 21, 2023 – Kampuni  ya michezo ya kubashiri, SportPesa kushirikiana na mtandao wa Tigo kupitia huduma ya TigoPesa leo asubuhi wamezindua kampeni inayoitwa ‘Maokoto Deilee’. Promosheni hii itawapa fursa watumiaji wa Tigo kuingia kwenye droo baada ya kuweka fedha zao kwenye akaunti zao za SportPesa, kupitia akaunti ya TigoPesa na kisha kuweka bashiri zao.

Keneth Ndulute kutoka Tigo Pesa, na Sabrina Msuya kutoka SportPesa

“Maokoto Deilee” inawapa nafasi wateja wa SportPesa na TigoPesa kujishindia zawadi za pesa kila siku, wiki pamoja na simu janja huku zawadi kubwa kabisa ikiwa ni kiasi cha shilingi 15,000,000 ambacho kitatolewa mwisho wa promosheni.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano SportPesa,Sabrina Msuya, alieleza kuwa, “ promosheni hii inampa nafasi kila mtumiahi wa mtandao wa Tigo kuweza kujishindia zawadi hata kama atakosa matokeo ya bashiri zake, mteja akishaweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kupitia TigoPesa na kuweka bashiri yake ,anapata fursa moja kwa moja ya kuingia kwenye droo ya wiki.  Wateja wetu wana fursa ya kujishindia zawadi za kila siku TZS 20,000/-, zawadi za wiki TZS 1m/- na zawadi kubwa ya TZS 15m/-.  Pia kila wiki washindi wawili wataweza kujinyakulia simu janja.

Akielezea kuhusu ushirikiano huo, Kenneth Ndulute, Meneja Biashara wa TigoPesa, alisisitiza kuwa, “kampeni hiyo ni fursa kwa wateja wa TigoPesa kufurahia na kushiriki promosheni hii ili kujishindia zawadi mbalimbali huku wakibashiri mechi wazipendazo kupitia mtandao wa Tigo. Ndulute aliwahimiza wateja kuchangamkia fursa hii na kushiriki katika kampeni ya “Maokoto, Deilee” ili waweze kujishindia zawadi hizi.”

Wateja wa TigoPesa ambao hawana akaunti ya SportPesa, wanaweza kufungua akaunti kwa kutembelea tovuti ya sportpesa au kupakua App ya SportPesa au kupiga code maalumu ya ussd sportpesa Baada ya kufungua akaunti,mteja anaweza akaweka fedha kwenye akaunti yake ya SportPesa kwa kutumia Tigopesa.

Ili kuweka bashiri yako kupitia TigoPesa, wateja wanaweza kupiga *150*87#, kuchagua namba 4, na kuweka kiasi anachotaka, kisha kuweka PIN yako ya Tigopesa ili kukamilisha muamala.

Ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi zinazotolewa kwenye promosheni ya ‘MAOKOTO DEILEE’ wateja wanahimizwa kuweka hela kwenye akaunti zao za SportPesa kupitia TigoPesa na kisha kuweka bashiri zao mara nyingi wawezavyo.

Chanzo: sportpesa blog tz