SHERIA YA BAHATI NASIBU YA TAIFA



[KANUNI]

INDEX TO SUBSIDIARY LEGISLATION

    KANUNI
        Kanuni za Bahati Nasibu ya Taifa

KANUNI
KANUNI ZA BAHATI NASIBU YA TAIFA

    Fungu
Mpango wa Mafungu Mbali Mbali

SEHEMU YA I
UTANGULIZI

    1.    Jina na mwanzo.
    2.    Tafsiri.

SEHEMU YA II
BAHATI NASIBU YA KAWAIDA

    3.    Kuendesha Bahati Nasibu za kawaida.
    4.    Wakati wa kucheza.
    5.    Idadi ya tikiti zitakazotolewa.
    6.    Zawadi za Bahati Nasibu za kawaida.

SEHEMU YA III
BAHATI NASIBU MAALUM

    7.    Bahati Nasibu Maalum.
    8.    Tikiti zita chanishwa kwa kila Bahati Nasibu Maalum.

    9.    Zawadi za Bahati Nasibu Maalum.
SEHEMU YA IV

TIKITI ZA BAHATI NASIBU
    10.    Bei ya tikiti.
    11.    Tikiti kupewa nambari zinazofuatana.
    12.    Tikiti zitatolewa katika vijitabu.
    13.    Yaliyomo ndani ya tikiti.
SEHEMU YA V
UUZAJI WA TIKITI ZA BAHATI NASIBU
    14.    Uteuzi wa Maajenti wauzaji.
    15.    Barua ya kuteuliwa.
    16.    Dhamana.
    17.    Utanguo Maajenti Uuzaji.
    18.    Ugawaji wa tikiti kwa maajenti wauzaji.
    19.    Tarehe za kwanza kuuza tikiti.
    20.    Tarehe za kufunga kuuza wa tikiti.
    21.    Uuzaji wa tikiti utakoma tarehe ya mwisho.
    22.    Wajibu wa kurejesha tikiti zote zilizouzwa pamoja na vishina siku ya mwisho.
    23.    Wajibu wa kulipa fedha taslimu kutokana na tikiti zote zilizouzwa.
    24.    Maajenti wadogo.
    25.    Jina la mnunuzi kuandikwa katika kishina cha tikiti.
    26.    Tikiti haitanunuliwa na zaidi ya mtu mmoja.
    27.    Namna ya kutunza vitabu vya hesabu.
    28.    Wizi wa tikiti.

SEHEMU YA VI
MICHEZO
    29.    Mahali pa kuchezesha mchezo.
    30.    Kamati ya kusimamia mchezo.
    31.    Kuahirisha mchezo.
    32.    Utaratibu.
    33.    Ukaguzi wa mashine.
    34.    Taksiri itokeapo wakati wa mchezo.
    35.    Tikiti zilizouzwa tu zishiriki katika kuchagua zawadi tatu za kwanza.
    36.    Tikiti inaposhinda zaidi ya zawadi moja.

SEHEMU YA VII
MADAI YA ULIPAJI WA ZAWADI
    37.    Tafsiri.
    38.    Wenye mamlaka ya kulipa.
    39.    Madai ya zawadi.
    40.    Tikiti zilizopotea.
    41.    Zawadi zisizodaiwa baada ya miezi sita.
    42.    Zawadi za wauzaji.

SEHEMU YA VIII
MIPANGO YA USALAMA

    43.    Tikiti zote zilizouzwa kuwekwa mahali pa usalama.
    44.    Kufungua vifurushi vya tikiti zisizouzwa.
    45.    Tikiti zisizouzwa zinazofika baada ya siku ya mchezo.
    46.    Kuharibu tikiti zisizouzwa.

SEHEMU YA IX
MAKOSA

    47.    Kushindwa kurejeshwa tikiti zisizouzwa.
    48.    Habari ya udanganyifu.
    49.    Kuharibu kifurushi chenye tikiti zisizouzwa.
    50.    Adhabu.

NYONGEZA
KANUNI

KANUNI ZA BAHATI NASIBU YA TAIFA
(Chini ya kifungu cha 20)

[1 Januari, 1978]
T.S. Na. 48 ya 1979

SEHEMU YA I
UTANGULIZI
1.    Jina la mwanzo
    Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Bahati Nasibu ya Taifa.
2.    Tafsiri
    Katika Kanuni hizi, mpaka iwapo maana nyingine itahitajika–
    "Bahati Nasibu" maana yake ni Bahati Nasibu ya Taifa;
    "Bahati Nasibu Maalum" maana yake ni Bahati Nasibu isiyo ya kawaida ambayo huendeshwa na kuchezeshwa na Mkurugenzi kwa kibali cha Bodi ili kuadhimisha sikukuu yoyote ile ya Taifa au siku ya mapumziko;
    "Bahati Nasibu ya Kawaida" maana yake ni Bahati Nasibu ambayo inaendeshwa na kuchezeshwa mara moja kila mwezi kwa kufuatana na vifungu vya Kanuni hizi;
    "Kamati" maana yake ni Kamati ya kusimammia Uchezeshaji ambayo imeteuliwa na Bodi chini ya Kifungu cha 30 cha Kanuni hizi;
    "Mamlaka ya ulipaji" maana yake ni mtu ambaye ameruhusiwa na Kanuni hizi kulipa zawadi kwa wenye tikiti zilizoshinda;
    "Sheria" maana yake ni Sheria ya Bahati Nasibu ya Taifa *;
    "tarehe ya mwanzo" maana yake ni tarehe ambayo uuzaji wa tikiti za Bahati Nasibu kwa ajili ya mchezo wowote ule wa Bahati Nasibu utaanza;
    "tarehe ya mwisho" maana yake ni tarehe ambayo uuzaji wote wa tikiti za Bahati Nasibu kwa ajili ya mchezo wowote ule wa Bahati Nasibu utakoma;
    "tikiti" maana yake tikiti ya Bahati Nasibu;
    "Utaratibu" maana yake ni tangazo ambalo limetolewa katika Gazeti la Serikali ambamo kuna habari kamili ambazo zinahitaji kutangazwa na Bodi kwa kufuatana na ibara ya (a) ya kifungu 7 cha Sheria ya Bahati Nasibu.

SEHEMU YA II
BAHATI NASIBU YA KAWAIDA
3.    Kuendesha Bahati Nasibu za kawaida
    Bodi itaendesha bahati nasibu ya kawaida mara moja kila mwezi.
4.    Wakati wa kucheza
    Mchezo wowote ule wa kawaida ambao utaendeshwa kila mwezi, kwa kufuata vifungu vya sehemu ya VI, utaendeshwa kati ya siku ya kwanza na ya ishirini na tano ya mwezi unaofuata, kama Mkurugenzi atakavyoamua.
5.    Idadi ya tikiti zitakazotolewa
    Mkurugenzi atachapisha tikiti kama itakavyoagizwa na Bodi kwa ajili ya kila mchezo wa Bahati Nasibu ya kawaida.
6.    Zawadi za Bahati Nasibu za kawaida
    Kutakuweko na zawadi zifuatazo katika kila mchezo wa kawaida wa Bahati ambazo zitatangazwa katika Gazeti la serikali na magazeti mengine kama itakavyoamriwa na Bodi:
    (a)    Zawadi ya Kwanza;
    (b)    Zawadi ya Pili;
    (c)    Zawadi ya Tatu;
    (d)    Zawadi ya Nne, zawadi mbili;
    (e)    Zawadi ya Tano, zawadi ishirini;
    (f)    Zawadi ya Sita, zawadi mia moja hamsini;
    (g)    Zawadi ya Saba, zawadi elfu moja na mia;
    (h)    Zawadi ya Nane, zawadi kumi na tano elfu.
SEHEMU YA III
BAHATI NASIBU MAALUM
7.    Bahati Nasibu Maalum
    (1) Pamoja na Bahati Nasibu za Kawaida Mkurugenzi anaweza kwa kibali cha Bodi, kuendesha Bahati Nasibu Maalum kuadhimisha sikukuu yoyote ya taifa au siku ya mapumziko.
    (2) Mchezo wa bahati Nasibu Maalum, kwa kufuatana na vifungu vya sehemu ya VI, utachezwa siku ambayo Mkurugenzi ataiweka katika utaratibu.
8.    Tikiti zitachapishwa kwa kila Bahati Nasibu Maalum
    Bodi itachapisha tikiti kwa idadi itakavyoamua, kwa ajili ya kila Bahati Nasibu Maalum.
9.    Zawadi za Bahati Nasibu Maalum
    (1) Bodi itaweka zawadi, katika kila mchezo wa Bahati Nasibu Maalum, ambazo zitatangazwa katika Gazeti la Serikali pamoja na magazeti mengine kama itakavyoamriwa na Bodi.
    (2) Bodi yaweza kubadili kima cha zawadi, kwa kutangaza katika Gazeti la serikali pamoja na magazeti mengine kama itakavyoonelea sawa katika kila Bahati Nasibu Maalum.

SEHEMU YA IV
TIKITI ZA BAHATI NASIBU
10.    Bei ya tikiti
    Bei ya kila tikiti kwa ajili ya bahati nasibu ya kawaida itawekwa na Bodi.
11.    Tikiti kupewa nambari zinazofuatana
    Tikiti zote zilizochapishwa kwa ajili ya bahati nasibu zitapewa nambari zinazofuatana kutoka nambari moja.
12.    Tikiti zitatolewa katika vijitabu
    (1) Tikiti zitatolewa katika vijitabu ndani yake zikiwamo tikiti ambazo idadi yake itakuwa kama itakavyoamua Bodi na kila tikiti itakuwa na kishina ambamo nambari itakayochapwa italingana na nambari ambayo itachapwa juu ya tikiti yenyewe ambayo pia iwe na nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuandika juu yake jina na anwani ya aliyenunua tikiti na jina na anwani ya muuzaji.
    (2) Jalada la kila kijitabu litakuwa limechapwa nambari ya kwanza na ya mwisho ya tikiti zilizomo katika kijitabu hicho na itakuwepo nafasi pia kwa ajili ya kuandika juu yake jina la muuzaji au mtu ambaye ameruhusiwa kuuza tikiti ambaye amepewa kijitabu hicho ili tikiti zilizomo ziuzwe.
13.    Yaliyomo ndani ya tikiti
   (1) Juu ya kila tikiti kutachapwa:
 (a)    nambari inayofuatana 
 (b)    bei ya tikiti

 

Chanzo :  https://tanzanialaws.com/sub-s/625-sheria-ya-bahati-nasibu-ya-taifa

Editor

I'm emanuel Masshele, experienced in igaming content writer, betting and casino review, igaming bussines, and affiliate marketing expert

Post a Comment

Previous Post Next Post