Jimmy
Masaoe, Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania (mwenye suti nyeusi)
akiwaongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kukata keki kama ishara ya
kuadhimisha mwaka mmoja wa Betway nchini Tanzania. Hafla ya maadhimisho
ya mwaka mmoja wa Betway Tanzania ilifanyika jioni ya Jumatano Julai 27
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubashiri Tanzania, James Mbalwe akizungumza
na washiriki wa hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa Betway Tanzania
(hawapo pichani). Mbalwe alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
iliyofanyika jioni ya Jumatano Julai 27 jijini Dar es Salaam.
Betway
inayomilikiwa na Super Group, ambayo ni kampuni maarufu ya kimataifa ya
ubashiri na bahati nasibu katika michezo mtandaoni imetimiza mwaka
mmoja tangu izinduliwe rasmi nchini Tanzania. Katika hafla fupi ya
kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo nchini Tanzania iliyofanyika
Jumatano Julai 27, 2022 jijini Dar es Salaam, Betway ilizindua huduma na
bidhaa mpya ikiwemo Betway Jackpot na jukwaa jipya la kubashiri
kidigitali.
Tangu
ilipoingia Tanzania, Betway imetekeleza mambo kadhaa makubwa ikiwemo
ukarabati wa viwanja vya michezo, ufunguzi wa kituo cha kisasa cha
kushuhudia michezo, pamoja na kuunda ushirikiano na mamlaka za michezo
na wadau ili kukuza maendeleo ya michezo nchini. Sambamba na hayo,
kampuni ya Betway imechangia katika uboreshaji wa sekta ya ubashiri na
michezo ya kubahatisha kwa kuanzisha huduma bora za kuwezesha ubashiri
kupitia majukwaa ya kidigitali.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo iliyowakutanisha zaidi ya wadau 50 wa sekta ya
ubashiri na michezo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, James Mbalwe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
aliipongeza kampuni ya Betway kwa jitihada za kukuza maendeleo ya
michezo nchini Tanzania na kuitaka kampuni hiyo kuendelea kuwa mfano
mzuri kwa makampuni mengine. Vilevile Mbalwe alitoa rai kwa Betway na
makampuni mengine ya ubashiri na michezo ya kubahatisha kuisaidia Bodi
hiyo katika utekelezaji kanuni na sera zinazolenga kukuza uwajibikaji
katika sekta ya ubashiri na michezo ya kubahatisha.
“Sekta
ya ubashiri na michezo ya kubahatisha kwa sasa inakua kwa kasi, katika
miongo miwili iliyopita ya kuanzishwa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
kumekuwa na upanuzi wa shughuli za ubashiri na michezo ya kubahatisha.
Ukuaji huu umechangia ongezeko kubwa la ukusanyaji wa mapato ambapo
sekta ya michezo ya kubahatisha ilipata ukuaji wa asilimia 20.69 katika
ukusanyaji wa ushuru wa michezo ya kubahatisha kutoka TZS 78.8 bilioni
mwaka 2017/18 hadi TZS 95.1 bilioni mwaka 2018/19. Haya ni mafanikio
makubwa ambayo hayawezi kupuuzwa. Mbali na hayo, sekta hii imeibua fursa
za ajira kwa Watanzania, imevutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka
nje, na kuchangia katika maendeleo ya teknolojia kupitia uhamishaji wa
teknolojia unaofanywa na makampuni haya yanapokuja kuwekeza Tanzania", alisema Mbalwe.
“Tunawapongeza
Betway kwa sababu katika kipindi cha mwaka mmoja wamefanikiwa kuweka
historia nzuri katika sekta ya ubashiri na michezo ya kubahatisha hasa
kwa kushika kibendera na kuendeleza dhana ya uwajibikaji katika
ubashiri, kuleta teknolojia za kisasa za kidigitali, kuanzisha mazingira
ya kisasa ya kushuhudia michezo, na muhimu zaidi kuchangia uboreshaji
wa miundombinu ya michezo. Haya ni mambo ya kupongeza, tunatumai kampuni
nyingine za ubashiri na michezo ya kubahatisha zitajifunza kupitia
Betway.” aliongeza Mbalwe.
Kwa
upande mwingine, Betway ilitumia fursa hiyo kutambulisha bidhaa zake na
huduma zake mpya ikiwa ni pamoja na Betway Jackpot, jukwaa jipya la
kubashiri kidigitali, mabalozi wapya, na kampeni mbili ambazo ni kampeni
ya Chomoka na Odds na nyongeza ya 700% kwa wateja wa kampuni hiyo.
Akizungumzia mwelekeo mpya uliotangazwa kampuni hiyo, Calvin Mhina
ambaye ni Meneja Masoko wa Betway Tanzania alisema.
“Kulingana
na utafiti wetu na uzoefu tuliokusanya katika kipindi cha mwaka mmoja,
tumekuja na bidhaa za kusisimua zaidi ambazo zitawafaa wateja wetu. Kwa
kuanza, tumezindua jukwaa jipya la kubashiri kwa urahisi zaidi
kidigitali ili kuwarahisishia huduma wateja wetu. Pia tumezindua jackpot
kubwa zaidi nchini yenye zawadi kubwa zaidi ya TZS 5,000,000,000, ili
kuwapa wateja wetu machaguo zaidi na uwezekano mkubwa zaidi wa kuboresha
maisha yao kupitia ubashiri na michezo ya kubahatisha. Hatua nyingine
kubwa ambayo tumefanya leo ni kuzindua odds mpya na kuongeza kiwango cha
ushindi kwa 700%. Tunatumai haya yataendekea kuongeza chachu ya
maendeleo ya sekta ya kamari nchini Tanzania.” alisema Mhina.
Kupitia
hafla hiyo iliyopambwa na huduma mbalimbali za kimichezo, Betway pia
ilitambulisha waraghibishi wawili wapya kwa lengo kukuza uhamasishaji wa
elimu ya kubashiri kistaarabu pamoja na huduma zinazotolewa na kampuni
hiyo. Waraghibishi wapya waliotambulishwa na Betway ni Priva Shayo
(Privaldihno) na George Ambangile - wote wawili ni watangazaji na
wachambuzi wa michezo.
Wadau
waliohudhuria hafla hiyo walifurahia huduma mbalimbali za michezo na
baadhi yao kujishindia zawadi za hadi TZS 100,000 kupitia mashindano
mbalimbali ya michezo yaliyokuwa sehemu ya hafla hiyo.
Kuhusu Betway Group
Betway
ni sehemu ya Super Group: kampuni ya kimataifa ya kidijitali ambayo
hutoa huduma ya daraja la kwanza ya kubashiri na bahati nasibu katika
michezo..
Super
Group (SGHC) Limited ni kampuni inayoongoza duniani katika biashara ya
kubashiri michezo mtandaoni na bahati na nasibu: Betway, chapa kubwa ya
kubashiri michezo mtandaoni na Kasino. Imeorodheshwa kwenye New York
Stock Exchange (NYSE ticker: SGHC), kampunii imepewa leseni katika
maeneo zaidi ya 20, ikiwa na nafasi za juu katika masoko makubwa kote
Ulaya, Amerika na Afrika.
Mafanikio
ya kikundi katika kubashiri michezo na bahati nasibu za mtandaoni
yanachagizwa na teknolojia nzuri ili kuiwezesha kuingia haraka na kwa
ufanisi katika masoko mapya. Teknolojia yetu husaidia katika upembuzi
yakinifu wa taarifa za masoko huiwezesha kutoa huduma za kipekee kwa
wateja. Kwa maelezo zaidi, tembelea www.sghc.com
Betway
Group ni mtoa huduma anayeongoza kwa huduma nzuri na ya kibunifu katika
kubashiri michezo, kasino na esports. Ilianzishwa mwaka wa 2006, na
inafanya kazi katika idadi ya masoko ya mtandaoni yaliyodhibitiwa.
Betway inajivunia kutoa huduma na bora kwa wateja wake inayochagizwa na
mazingira rafiki, salama, haki na uwajibikaji.
Betway
ni mwanachama wa taasisi kadhaa katika tasnia, ikiwemo International
Betting Integrity Association (IBIA), iGaming European Network (iGEN),
Independent Betting Adjudication Service (IBAS), Sports Wagering
Integrity Monitoring Association (SWIMA) na Betting na Gaming Council
(BGC), na inatambuliwa kwa ISO 27001 kupitia wakala wa vipimo na viwango
anayeaminika wa kimataifa eCOGRA.
Betway
Tanzania, inasimamiwa na Media Bay Limited imepewa Leseni na kusimamiwa
na Wizara ya Fedha na Mipango, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya
Tanzania.
0 Comments