Mpesa nimiongoni mwa huduma inayotumika katika kutoa na kuweka pesa kwenye kampuni za kubeti

Utangulizi 

Huduma za kifedha za simu za mkononi no huduma zitolewazo na makampuni ya simu za mkononi ambapo huwezesha kutiririka kwa miamala ya kifedha kutoka kwa mtu mmoja na mwingine kwa mpangilio wa kiutoaji na upokeaji. Mfano wa huduma za kifedha za simu za mkononi kwa Tanzania ni M-PESA, Tigo pesa, Airtel money, na halopesa. Kampuni za betting ni kampuni zinazojihusisha na kuendesha michezo ya bahati nasibu Tanzania.

Kwa njia nyingi za kiafrika hasa mataifa yanayoendelea watumiaji wake huweza kufikia huduma za malipo kwa njia ya simu za mkononi katika kutoa na kuweka pesa katika kampuni za betting uliko njia nyingine za malipo Kama vile malipo kwa njia ya bank, fedha za kidigitali, na njia nyingine za malipo kwa njia ya mtandao.

Kwa Tanzania kulingana na utafiti uliofanywa na mtandao huu watoa huduma wa michezo ya ubashiri mtandaoni hutumia njia za malipo ya simu za mkononi Kama vile M-PESA, Airtel money, Tigo pesa na halopesa. 

SOMA PIA: KAMPUNI ZA KUBETI TANZANIA

Hivyo tunaweza kusema kuwa kuwepo kwa huduma hizi kumechochea na kunawirisha biashara hii inayokuwa kwa Kasi duniani.

Changamoto zilizopo

Pamoja na faida lukuki za kutumia njia rahisi za malipo ya huduma za malipo ya kifedha kwa njia ya simu za mkononi changamoto kubwa iliyopo ni, pamoja na Makato makubwa pamoja  katika kutuma miamala(deposits) na Makato wakati wa utoaji fedha. Changamoto nyingine iliyopo ni pamoja na changamoto ya kuchelewa kwa miamala kunakoripotiwa kujitokeza Mara kadhaa. 

Pamoja na hayo makampuni ya simu za mkononi yanayo nafasi kubwa ya kuboresha huduma kwa watumiaji wake ili kuzidi kunawirisha tasnia ya michezo ya bahati nasibu tanzania