Serikali imeongeza kiwango cha kodi kwa washindi wa michezo ya kubashiri (Betting) ambapo Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema Ongezeko la kiwango hiko cha fedha kitakachopatikana, asilimia 70 itaenda katika mfuko wa serikali kupambana na Ukimwi na asilimia 30 kuchangia mfuko wa bima ya afya.
“Kufanya marekebisho kwenye sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41. Kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15,” amesema Waziri Mwigulu Nchemba bungeni Dodoma leo wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026. ✍️